Social Icons

Featured Posts

Wednesday, March 30, 2016

Monday, February 15, 2016

RUVUMA TV: HII HAPA ILE STORY YA DEREVA BODA BODA KUUWAWA NA WATU WASIOJULIKANA SONGEA

Dereva boda boda aliejulikana kwa Jina VICTOR NJIWA mkazi wa Bombambili Mjini Songea mkoani Ruvuma amekutwa ameuwawa na watu wasio julikana na mwili wake kuokotwa pembeni mwa barabara kuu Songea, Njombe ukiwa ulelazwa katika mtaro wa maji.

Saturday, February 13, 2016

Mwanamke Aliyepambana na Kunyang’anya Bunduki Jambazi Azawadiwa Laki 5

RISASI MAJAMBAZI MWANAMKE (4)Sophia Manguye akisaini mara baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo.

Mwanamke aliyepambana na jambazi na kufanikiwa kumnyang’anya bunduki aina ya SMG, Sophia Manguye (46), amepewa zawadi ya Sh 500,000 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Tarime/Rorya, Gemini Mushy.
Mwanamke huyo ambaye aliomba Serikali kumpa silaha ili kujilinda, alisema kuwa hajaridhika na zawadi hiyo kwa kuwa kama asingemmudu jambazi huyo watu wengi wangepoteza maisha.
Hata hivyo, Mushy alimwomba Manguye kupokea kiasi hicho japokuwa ni kidogo kwa kuwa ni zawadi kutoka ofisi yake.
Tukio hilo lilitokea Februari 9, saa 2.42 usiku, baada ya watu watatu kufika dukani kwake, mmoja wao akiwa na bunduki kisha kumwamuru atoe fedha alizokuwa nazo.Manguye alisema alichukua Sh80,000 alizokuwa nazo na kumkabidhi jambazi huyo, lakini hakuridhika na kumlazimisha aongeze kiasi kingine.“Nilipandwa hasira nikanyanyuka wakati jambazi anainama kuangalia kwenye kiboksi cha fedha, nikamkamata kifuani na kung’ang’ania mkanda wa bunduki, akaanza kunivuta kwenda nje, nami nikamvutia ndani, lakini alifanikiwa kunitoa nje akaniangusha chini, lakini sikuachia mkanda wa bunduki,” alisema Manguye na kuongeza: “Aliposikia wananchi wameanza kupiga yowe akaniachia na kutoa mkanda wa silaha begani, akakimbia na kuniachia bunduki. Wakati huo huo jambazi mwingine alikuwa amekamatwa kwenye duka la Zaituni Magasi, wananchi walipofika wakaanza kumshambulia, wakati huo taarifa ilikuwa tayari imetolewa Kituo cha Polisi Sirari, wakafika kumchukua,” alisema. Hii ni mara ya pili kwa Manguya kuvamiwa na majambazi wenye silaha, ambapo mwaka 2014 alivamiwa dukani kwake na majambazi waliokuwa na bunduki, lakini alifanikiwa kumpiga kwa kigoda aliyekuwa na bunduki na alianguka chini.Magasi alisema wakati wa tukio hilo, alikuwa amevamiwa na majambazi waliokuwa na bunduki, mapanga na nondo.“Wakati anatoka mvunguni mdogo wangu alimkamata kwa nyuma na kummudu huku akipiga kelele, watu wakafika wakaanza kumpiga hadi akazimia, polisi walipofika wakamwokoa kwani kidogo wamuue,”alisema.

MABONDIA MKOA WA RUVUMA “ Mh. NAPE MOSES NNAUYE TUTUMBULIE JIPU CHAMA CHA NGUMI MKOA WA RUVUMA VIFAA VYA THAMANI YA MILIONI 7 VYA UZWA

Tuesday, December 15, 2015

IAWRT YAZINDUA RIPOTI YA NAFASI YA MWANAMKE KATIKA VYOMBO VYA HABARI

Bi Razia Mwawanga kutoka IAWRT akifungua mkutano wakati wa uzinduzi wa ripoti ya utafiti kuhusu wanawake wanavyopewa nafasi hasa katika vyombo vya habari hasa hapa nchini.(Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja blog)

UNODC YAKABIDHI VIFAA VYA MAABARA JESHI LA MAGEREZA

MADIWANI NA WATAAKAMU RUVUMA WATAKIWA LIWATUM,IKIA WANANCHI KWA UADILIFU

 
Mkuu wa mkoa wa ruvuma Said Mwambungu akisisitiza jambo.
Na Nathan Mtega,Songea

Madiwani na wataalamu wa halmashasuri za wilaya na manispaa mkoani Ruvuma wametakiwa kusimamia ukusanyaji wa mapato na kudhibiti matumizi yanayokusanywa na kujitambua kuwa wao ni wawakilishi wa wananbcvhi na wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia weledi.

Wednesday, November 18, 2015

FAHAMU JINSI #RECRUITME INAVYOWEZA KUKUPA UJUZI UTAKAOKUSAIDIA KUPATA KAZI UITAKAYO


Ujuzi, katika soko la ajira ni mali ambayo inahitaji matengenezo na uboreshaji. Kama mali nyingine yoyote, matumizi yake bora, hukuzalishia zaidi. Sababu nyingi zimetolewa katika kipindi cha miaka mingi kwamba kuna utofauti wa wazi baina ya mtu mwenye elimu aliyeko kazini na mwenye elimu bila kazi. Utofauti huo ni jinsi ujuzi wa watu hao wawili unavyotumika.

SHUJAAZ RADIO SHOW NA DJ TEE KUANZA KURUKA HEWANI KUPITIA EAST AFRICA RADIO.

Unamkumbuka yule dogo aliyeanzisha redio stesheni yake nyumbani kwao? Bila shaka umewahi kusoma story yake kwenye kijarida cha kila mwezi kiitwacho SHUJAAZ ambacho husambazwa na gazeti la Mwanaspoti na vibanda vya Coca Cola. Sasa hivi, dogo ana habari mpya na njema kwa vijana na wote  wanaomfuatilia. Nyota imeanza kung’ara upande wake na sasa redio kubwa Tanzania EAST AFRICA RADIO imeamua kumpa nafasi aweze kusikika hewani na show yake mpya iitwayo SHUJAAZ.

“Show yangu itahusika na lifestyle ya vijana kwa ujumla, bila kusahau burudani kali, story za wana mbali mbali wanaojituma na kutoboa katika kufikia malengo yao maishani. Pia, utawasikia vijana mbali mbali wakijadiliana kuhusu ishu zinazowahusu, mfano PESA, MAPENZI, KAZI, MICHEZO, UJASIRIAMALI n.k, ni lazima tupeane mashavu kama vijana.” Alisema DJ Tee.

Show hiyo itakayoanza rasmi JUMAMOSI hii (07/11/2015) saa TISA alasiri, inatarajiwa kuvuta hisia za vijana wengi hasa wajasiriamali kwa kuwa itahusika na ishu zote ambazo zinawahusu vijana kama DJ TEE mwenyewe alivyoelezea.
Unaweza kupata maelezo zaidi kutoka kwake mwenyewe kwa kujiunga naye kupitia Facebook jina ni DJ Tee (http://on.fb.me/1FUl1hX), Twitter (http://bit.ly/1LLGEpK) na Instagram (http://bit.ly/1Hn07t4

Tuesday, November 3, 2015

MSIMAMIZI WA PROGRAMU YA AFRICAN DREAM KUTOKA SHIRIKISHO LA MCHEZO WA WAVU AFRIKA (CAVB) ATEMBELEA WIZARA YA HABARI

ima1
Msimamizi  wa Programu ya “African Dream” kutoka  CAVB ( Shirikisho la Mchezo wa Mpira wa Wavu Afrika) Paul Bitok  wa pili kutoka kulia akimuuliza jambo Katibu Mtendaji wa Chama cha Mpira wa Wavu nchini ( TAVA)  Bw. Allen Alex alipotembelea Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo  kujadiliana juu ya  maendeleo ya mchezo huo nchini,Wa kwanza kutoka kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Olimpiki Tanzania Bw. Muharam Mchume  Picha na Benjamin Sawe
ima2
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi Juliana Yassoda wa pili kutoka kushoto akimuelezea  Msimamizi  wa Programu ya “African Dream” kutoka  CAVB ( Shirikisho la Mchezo wa Mpira wa Wavu Afrika) Paul Bitok  jinsi Serikali inavyoshirikiana na Chama cha Mpira wa Wavu nchini katika kukuza mchezo huo.Picha na Benjamin Sawe
ima3
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Olimpiki Tanzania  Bw. Muharam Mchume wa kwanza kushoto akimuelezea  Msimamizi  wa Programu ya “African Dream” kutoka  CAVB ( Shirikisho la Mchezo wa Mpira wa Wavu Afrika) Paul Bitok  wa pili kutoka kulia jinsi wanavyoshirikiana  na Serikali katika kukuza mchezo huo.Msimamizi yupo nchini kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya mchezo huo. Picha na Benjamin Sawe

NAIBU KATIBU MKUU MPYA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AANZA KAZI RASMI NA KUWATAKA WATUMISHI KUTEKELEZA KAULI MBIU YA “HAPA KAZI TU”

nd1
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi aliyeteuliwa hivi karibuni, John Mngodo, akijitambulisha kwa Watumishi  mara baada ya kuanza kazi rasmi  katika Wizara hiyo. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Lilian Mapfa na kushoto ni Mwenyekiti wa TUGHE,  Obedi Mbaga.
nd2
Mkurugenzi wa Idara ya Sheria katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Marlin Komba akijitambulisha mbele ya Naibu Katibu Mkuu mpya, John Mngodo (hayupo pichani) wakati wa Mkutano kati ya Watumishi na Naibu Katibu Mkuu huyo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara.
nd3
Naibu Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, akizungumza na Watumishi mara baada ya kuanza kazi rasmi katika Wizara hiyo.
nd4
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu mpya wa Wizara (hayupo pichani) alipofanya mkutano na watumishi hao mara baada ya kuanza kazi rasmi katika Wizara hiyo.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI WILLIAM LUKUVI AAGA RASMI SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akipokea ngao yenye picha ya chui ikiwa ni ishara ya tuzo ya Shirika la Nyumba la Taifa kwa Waziri huyo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu kwa kuonyesha utendaji uliokuwa wa kasi usiochoka wakati Waziri Lukuvi alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi.
Waziri wa ArdhiNyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akipokea ngao yenye picha ya chui ikiwa ni ishara ya tuzo ya Shirika la Nyumba la Taifa kwa Waziri huyo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu kwa kuonyesha utendaji uliokuwa wa kasi usiochoka wakati Waziri Lukuvi alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi.
Waziri wa ArdhiNyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akipokea kadi ya pongezi ya Shirika la Nyumba la Taifa kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii, Susan Omari kwa kuonyesha utendaji uliokuwa wa kasi usiochoka wakati Waziri Lukuvi alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza na Wakurugenzi na Mameneja wa Makao Makuu ya Shirika hilo wakati Waziri Lukuvi alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi.
Baadhi ya mameneja wa Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wakifuatilia mazungumzo wakati Waziri Lukuvi alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza na Wakurugenzi na Mameneja wa Makao Makuu ya Shirika hilo wakati Waziri Lukuvi alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi.
  Waziri Lukuvi akizungumza na Wakurugenzi na Mameneja wa Makao Makuu ya Shirika hilo wakati alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu.
 Waziri Lukuvi akizungumza na Wakurugenzi na Mameneja wa Makao Makuu ya Shirika hilo wakati alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu.
Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, Fatma Chillo akizungumza kwa niaba ya Wakurugenzi na Mameneja wa Makao Makuu ya Shirika hilo kumshukuru Waziri huyo wakati Waziri alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi.
Waziri wa ArdhiNyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi ameiagiza Menejimenti ya Shirika hilo kuhakikisha inaendeleza kasi ya ujenzi wa nyumba za makazi na biashara bila kusahau misingi iliyoliunda shirika hilo.
Akizungumza leo wakati akiaga rasmi Shirika hilo alisema amejifunza mengi katika uwepo wake ndani ya Wizara na hasa dhamira na utendaji wa kasi wa Shirika hilo na akaiagiza menejimenti ya Shirika hilo kufanya kazi bila kuchoka likihakikisha linapigania makazi bora kwa kila mtanzania.
“Kabla ya kuingia katika Wizara , na hata nilipoingia sikuwa nafahamu kwa kina kwamba Shirika la Nyumba limebadilika kutoka lile la kuangalia nyumba za msajili wa majumba na kuwa sasa limejenga nyumba nyingi na kuziuza kwa Watanzania, sasa nimefahamu kwa kujifunza kwamba Shirika letu hili limebuni utaratibu unaolifanya lifanye kazi kwa kasi kubwa kibiashara lakini pia likibakia na ‘human face’, “alisema Lukuvi.
Alisema Serikali inafahamu changamoto linazokabiliana nazo Shirika hilo za ulipaji wa VAT mara mbili na gharama za miundombinu kama maji, umeme na barabara ambazo mara kadhaa zimekuwa zikirudi kwa mnunuzi wa mwisho na kwamba zinafanyiwa kazi pia akaliagiza Shirika na mamlaka hizo kukaa pamoja na kuweka mipango yao pamoja  ili angalau kuliwezesha Shirika kuwafikia Watanzania wengi.
Waziri Lukuvi alisema kuwa Serikali inaitambua sekta ya nyumba kuwa ni sekta mtambuka kwa kuwa hukuza uchumi, huongeza ajira na kusaidia kudumisha amani ya nchi yetu. Hivyo, alilihimiza Shirika hilo liendelee na mipango yake kabambe ya kujenga nyumba za gharama nafuu ili kuwawezesha wananchi wengi kumiliki nyumba.
Alisema wananchi wengi wakimiliki nyumba utakuwa mkakati mmojawapo wa kupunguza umaskini nchini maana wananchi hao wataweza kutumia nyumba zao kupata mikopo benki ya kuendeleza shughuli zao za kiuchumi.
Akiungumzia Serikali ya awamu ya Tano ijayo alisema kama kuna watumishi wa umma ambao walikuwa wakifanya mambo kwa mazoea katika awamu zilizopita basi awamu hii wahakikishe wanakuwa mguu sawa kwani Serikali ya Magufuli ambayo inaingia madarakani ni serikali isiyotaka mchezo wala lele mama na kwamba wala rushwa, na wazembe watatafuta mlango wa kutokea.
Akimkaribisha Waziri Lukuvi, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu alisema Shirika hilo linatekeleza miradi yake ili kuhakikisha linaweka makazi bora kwa Watanzania 
Alisema kwa shirika hilo lonafanya hivyo kwa kuwa sekta ya nyumba ni sekta mtambuka katika maendeleo ya uchumi. Sekta ya nyumba husaidia kuleta maendeleo ya haraka ya sekta zinginena kutoa ajira. Taifa linalozingatia sekta ya nyumba huwezesha nchi yao kuwa na amani, kwani mtu mwenye makazi bora, huthamini uwepo wa amani. 

MHUBIRI MAARUFU DUNIANI TB JOSHUA WA NIGERIA ATUA DAR ES SALAAM KUSHUHUDIA DKT MAGUFULI AKIAPISHWA

Mtume TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations nchini Nigeria  ametua jijini Dar es salaam leo  tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.
Mara tu baada ya kutua uwanja wa Ndeghe wa Kimataifa wa Julius Nyerere, TB Joshua alikwenda Ikulu moja kwa moja kumsalimia Rais Jakaya Mrisho  Kikwete  kumsabahi na kumpongeza kwa kufanikisha uchaguzi mkuu kwa uhuru na amani, huku akiondoka madarakani akiwa mtu mwenye furaha. TB Joshua amepongeza Rais Kikwete pia kwa kupata Dkt Magufuli kama mrithi wake, akimtaja Rais huyo mpya mteule kama Rais wa Tanzania wa Baraka na Fanaka tele katika awamu hii mpya.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Mtume TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations la nchini Nigeria Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii. TB Joshua ametua jijini Dar es salaam  tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mtume TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations la nchini Nigeria Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii.
Picha na Freddy Maro

USTAHIMILIVU WA VILABU KATIKA EPL NA MBIO ZA KUWANIA UBINGWA WA LIGI HIYO KATIKA MSIMU WA 2015/2016


Na Oswald Ngonyani.
Ligi Kuu ya England imekwishafikia katika raundi ya 11 huku vilabu kadhaa vikionekana kudhamiria kuutwaa ubingwa huo, hii ni kutokana na jinsi vinavyovuna pointi tatu muhimu karibu katika kila mchezo.

Tofauti na mpambano wa ligi zilizopita, msimu huu timu kadha wa kadha zinaonekana kuchuana kweli kweli kwa lengo la kuhakikisha kuwa zinafanya kile ambacho wenye timu lakini pia mashabiki wanapenda kifanyike.

Mpaka sasa zimebaki raundi nane ili kuweza kuhitimisha mechi za mzunguko wa kwanza sawa na raundi 27 ili kuhitimisha mzunguko mzima wa Ligi na hata kuweza kumtangaza mshindi. Zifuatazo ni timu sita bora ambazo kwayo mmoja wao atakuwa bingwa wa EPL 2015/2016.

Manchester City:
Wachezaji wengi wa kikosi hiki cha Manuel Pellrgrin wapo katika ubora wao kwa sasa, Waingereza hupenda kusema  ‘On fire’. Uwepo wa akina Sergio Kun Aguero, Rahim Sterling, na hata De Broyne ni vitu vinavyozidi kuchagiza ubora wa kikosi hicho kwa sasa.

Ni kikosi kinachoongoza Ligi baada ya kushuka dimbani mara 11 huku kikiwa na hazina ya pointi 25 sawa na Arsenal lakini kikiwa na mtaji mkubwa wa magoli. Uwepo wa walinzi wenye uwezo wa kufunga kama akina Vincent Kompany ni kitu kingine kizuri zaidi kinachozidi kuchagiza ukulu wa kikosi hicho.

Kwa sasa kinapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa EPL 2015/2016, jambo ambalo ni la msingi mno kwa mabosi wa timu hiyo lakini pia mashabiki wa kikosi hicho hasa baada ya kushindwa kuutetea ubingwa huo katika msimu uliopita.


Arsenal:
Kwa muda mrefu sasa Washika bunduki hawa wapo katika shauku kubwa ya kuuwinda ubingwa wa EPL baada ya kushindwa kuutwaa kwa zaidi ya miaka kumi sasa.
Kila mwanafamilia wa timu hiyo ana hamu ya kufanya hivyo, na kwa kila hali msimu huu unaonekana kuwaendea vizuri zaidi pengine kuliko misimu mingine yote iliyopita.

Ni wazi kuwa Arsene Wenger anajua nini kinatamaniwa zaidi na mabosi na mashabiki wa timu hiyo kwa sasa. Pamoja na kutwaa ndoo ya FA mara mbili mfululizo bado haijawa sababu ya wafuasi wa kikosi hicho kuridhika, bado wanautaka ubingwa wa EPL.

Pengine ustahimilivu wa kikosi hicho kwa sasa ni mojawapo ya vitu vya msingi zaidi vinavyowapa imani mashabiki wengi wa kikosi hicho kuamini kuwa mwaka huu ni mwaka wao wa kufanya makubwa katika soka ya England, yaani kuitwaa ndoo ya EPL.

Hapana shaka umakinifu wa akina Alexis Sanchez, Giroud na hata Mesut Ozil ni vitu vya msingi zaidi vinavyoipambanua Arsenal ya sasa na hata kuiweka katika mazingira salama zaidi ya kutwaa ubingwa huo.
Mpaka sasa washika mitutu hawa wanashika nafasi ya pili nyuma ya Manchester City kwa utofauti wa magoli ya kufunga na kufungwa baada ya wote kwa pamoja kulingana pointi.


Manchester United:
Mashetani hawa wekundu wangali wana hasira ya kuwa katika kipindi ambacho kwao kitaendelea kukumbukwa milele. Tangu Mzee Fergusson alipostaafu kuifundisha timu hiyo, timu hiyo imeonekana kukumbwa na upepo mkali, upepo ambao kwa msimu huu umeonekana kutulia.

Hakuna kitu kingine kinachowazwa na Wamiliki lakini pia mashabiki wa klabu hiyo kwa sasa zaidi ya ubingwa wa EPL. Mpaka sasa kikosi hicho kinashika nafasi ya nne kikiwa na hazina ya pointi 21, pointi nne nyuma ya vinara wa Ligi hiyo Manchester City, Arsenal, lakini pia pointi moja nyuma ya Leicester City.
Uwepo wa akina Depay,Martial A, na hata Juam Mata ni vitu vinavyozidi kuiweka Manchester United katika ubora wake na hata kutishia kinyang’anyiro cha kuuwania ubingwa huo mkubwa wa Ligi nchini England.


Tottenham:
Kikosi hiki kipo katika ubora wa hali ya juu kwa sasa japo hakipewi nafasi kubwa ya kuibuka bingwa wa EPL 2015/2016. Pengine mazoea ya vilabu fulani fulani kutwaa ndoo hiyo ndiyo sababu ya timu hiyo kutopewa nafasi.

Kikosi hiki kinashika nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi nyuma ya Man City, Arsenal,Leicester City, na Man U. Uwepo wa akina Harry Kane lakini pia Dembele M. ni miongoni mwa sababu zinazoiweka Tottenham katika vita hiyo ya ubingwa wa EPL 2015/2016.

Liverpool:
Pamoja na kukumbwa na wimbi zito la ukame wa vikombe bado ninaiwela Liverpool katika mbio hizi za ubingwa wa EPL 2015/2016.

Umakinifu wa kocha Brendan Rodgers lakini pia uwepo wa akina Coutinho na Christian Benteke pale Anfield ni vitu ambavyo kwayo vimesaidia kuifanya Liverpool ya leo iwe Liverpool. Msimu wa 2013/2015 ulionekana kuwa na tija zaidi kwa kikosi hicho lakini kwa bahati mbaya kikaishia kushika nafasi ya pili nyuma ya Manchester City.

Chelsea:
Pengine nitashindwa kueleweka na wengi kuhusu kuiweka Chelsea katika kinyang’anyiro hiki cha kuelekea ubingwa wa EPL 2015/2016. Lakini binafsi nitaendelea kuamini tena na tena kuwa Mourinho bado ana nafasi ya kutetea ubingwa wake ingawa kibarua chake kipo shakani.

Kikosi hiki chenye pointi 11 kipo babaikoni kwa sasa huku shauku ya mashabiki wake wengi ikimtaka Bosi wa timu hiyo kusitisha kandarasi ya mkufunzi wake, Mreno Jose Antonio Mourinho.

Chelsea ndiyo mabingwa watetezi wa EPL lakini ustahimilivu wake kwa sasa umeonekana kujenga shaka kwa wengi. Chelsea hii ya leo siyo ile tuliyokuwa tumeizoea. Mwenendo wake katika ligi umeonekana kutia shaka na hata kuzidi kuleta hofu kwa wenye unasaba na timu hiyo.

Kimahesabu ya mpira, Vijana hawa wa darajani bado wana nafasi ya kuitwa ndoo hii ya EPL kwa msimu huu 2015/2016 lakini hii itategemea zaidi na kile kitakachofanywa na timu zilizo kileleni kwani michezo 27 iliyobaki ni mingi sana, na chochote kinaweza kutokea mbele ya safari.
Nawasilisha hoja
(0767 57 32 87)


 
 
Blogger Templates