Social Icons

Sunday, January 13, 2013

JESHI LA ZIMAMOTO LATOA ELIMU YA KUKABILIANA NA JANGA LA MOTO SONGEA

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabiti Mwambungu
Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Ruvuma Baraza Mvano
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabiti Mwambungu akizima moto
 Mashauli wa Mgambo mkoa wa Ruvuma Kanali Fula akizima moto
 Mwandishi wa Habari akizima Moto
 Askari wazima moto wakizima moto
 Askari wa zima moto wakijadili namna ya kuendesha zoezi hilo la kuwasha moto na kuzima
 
Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Ruvuma  limetoa elimu kwa wananchi juu ya kukabiliana na majanga ya moto katika sehemu za kazi, majumbani na mashambani. 
Elimu hiyo imetolewa kwa vitendo ambapo watu mabalimbali waliongozwa na mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabiti Mwambungu  namana ya kutumia vifaa vya kisasa kuzima moto wenye kuleta madhara .

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw.Said Thabiti Mwambungu akatumia nafasi hiyo kuwataka wale wote wenye tabia za kuchoma moto barabarani na kwenye makazi ya watu waache  mara moja. Kwani uchomaji wa moto ni uhalibifu  wa mazingira na usababisha madhara makubwa sana hivyo serikali haitawafumbia macho.

Pia amewaomba wananchi wawafichue wale wote wenye tabia hizo sababu wanawafahamu hivyo wasiwaogope kuwafichua ili kukomesha majanga haya ya moto
Kutokana na majukumu hayo Kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani hapa BARAZA MVANO amesema jeshi hili limelazimika kutoa elimu ya kukabiliana na majanga ya moto kwa kuwa wanachi wanapopatwa na mataizo ya kuunguliwa nyumba ama mali zao hawatoi taarifa kwa wakati.

Kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoji  Baraza mvano amesema jeshi hilo limejiwekea mikakati ya kuelimisha wananchi katika wilaya zote tano za mkoa wa Ruvuma namna ya kuzima moto ili kupunguza madhara ya moto na wananchi kuelewa majukumu ya jeshi hilo.

Post a Comment
 
 
Blogger Templates